sw_tn/act/14/03.md

40 lines
1.3 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Maelezo ya jumla
Hapa neno "Yeye" linamaanisha Bwana.
# Kwa hiyo wakabaki kule
"Hata hivyo walibaki kule." Paul na Barnaba walibaki ikonia kuwasaidia watu wengi walioamini katika 14:1. "Kwa hiyo" inaweza kuondolewa kama itaongeza mchanganyiko kwenye maandishi.
# kutoa uthibitisho kuhusu ujumbe wa neema yake
"kuonesha kwamba ujumbe kuhusu neema yake ni kweli"
# kuhusu ujumbe wa neema yake
"kuhusu ujumbe wa neema ya Bwana"
# kwa kuruhusu ishara na maajabu kufanywa na mikono ya Paulo na Barnaba.
HIi inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kwa kuwawezesha Paulo na Barnaba kufanya ishara na maajabu"
# kwa mikono ya Paulo na Barnaba
Hapa "mikono" inamaanisha nia na juhudi za wanaume hawa wawili kulingana na walivyoongozwa na Roho Mtakatifu. "kwa huduma ya Paulo na Barnaba"
# sehemu kubwa ya mji uligawanyika
Hapa "mji" inamaanisha watu waliomo kwenye mji. "watu wengi wa mji waligawanyika" au "watu wengi wa mji hawakukubaliana"
# walikuwa upande wa wayahudi
"waliaunga mkono Wayahudi" au "walikubaliana na Wayahudi." Kundi la kwanza lililotajwa halikukubaliana na ujumbe kuhusu neema.
# na mitume
Kundi la pili lililotajwa lilikubaliana na ujumbe kuhusu neema. Inaweza kusaidia kutaja tena kitezi. "walijiunga na mitume"
# mitume
Luka anamaanisha Paulo na Barnaba. Hapa "mitume" inaweza kutumika katika hali ya ujumla ya "wale waliotumwa nje."