# Maelezo ya jumla Hapa neno "Yeye" linamaanisha Bwana. # Kwa hiyo wakabaki kule "Hata hivyo walibaki kule." Paul na Barnaba walibaki ikonia kuwasaidia watu wengi walioamini katika 14:1. "Kwa hiyo" inaweza kuondolewa kama itaongeza mchanganyiko kwenye maandishi. # kutoa uthibitisho kuhusu ujumbe wa neema yake "kuonesha kwamba ujumbe kuhusu neema yake ni kweli" # kuhusu ujumbe wa neema yake "kuhusu ujumbe wa neema ya Bwana" # kwa kuruhusu ishara na maajabu kufanywa na mikono ya Paulo na Barnaba. HIi inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kwa kuwawezesha Paulo na Barnaba kufanya ishara na maajabu" # kwa mikono ya Paulo na Barnaba Hapa "mikono" inamaanisha nia na juhudi za wanaume hawa wawili kulingana na walivyoongozwa na Roho Mtakatifu. "kwa huduma ya Paulo na Barnaba" # sehemu kubwa ya mji uligawanyika Hapa "mji" inamaanisha watu waliomo kwenye mji. "watu wengi wa mji waligawanyika" au "watu wengi wa mji hawakukubaliana" # walikuwa upande wa wayahudi "waliaunga mkono Wayahudi" au "walikubaliana na Wayahudi." Kundi la kwanza lililotajwa halikukubaliana na ujumbe kuhusu neema. # na mitume Kundi la pili lililotajwa lilikubaliana na ujumbe kuhusu neema. Inaweza kusaidia kutaja tena kitezi. "walijiunga na mitume" # mitume Luka anamaanisha Paulo na Barnaba. Hapa "mitume" inaweza kutumika katika hali ya ujumla ya "wale waliotumwa nje."