sw_tn/2jn/01/01.md

44 lines
1.2 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Sentensi Unganishi
Baada ya salamu, Yohana anawaonyesha waumini kuwa upendo na kweli vinakwenda sambamba
# Maelezo ya Jumla
Kihistoria mtume Yohana amekubalika kuwa ndiye mwandishi wa barua hii. Anasema "pendaneni" hii pengine barua hii liliandikiwa kanisa.
# Maelezo ya Jumla
"ninyi" na "yenu" katika barua hii yanaonyesha wingi
# Maelezo ya Jumla
katika barua hii Yohana anatumia maneno "sisi" na 'yetu" ikimaanisha Yohana mwenyewe pamoja na wasomaji wake
# Kutoka kwa mzee kwenda kwa mwanamke mteule na watoto wake
Barua za wakati huo zilianza na jina la mwandishi, kwa kushupisha inaweza kusomeka:- " mimi, Yohana mzee, ninaandika barua hii kwa mwanamke mteule na watoto wake"
# Mzee
Ni rejea kwa Yohana, mtume na mwanafunzi wa Yesu. Anajiita mzee labda kwa sababu ya umri wake mkubwa au kwa sababu ni kiongozi kanisani.
# kwa mwanamke mteule na watoto wake
Pengine hii ina maana ya kundi au kusanyiko na waumini .
# ambaye nampenda katika kweli.
" Ninyi watu ninaowapenda katika kweli"
# wanao ifahamu kweli
"ambao wanao fahamu ukweli kuhusu Mungu na Yesu"
# Baba...Mwana
Hivi ni vyeo muhimu vinavyoelezea uhusiano kati ya Mungu na Yesu
# katika kweli na upendo.
Neno "kweli" linaelezea "upendo." Pengine inamaanisha "katika upendo wa kweli"