# Sentensi Unganishi Baada ya salamu, Yohana anawaonyesha waumini kuwa upendo na kweli vinakwenda sambamba # Maelezo ya Jumla Kihistoria mtume Yohana amekubalika kuwa ndiye mwandishi wa barua hii. Anasema "pendaneni" hii pengine barua hii liliandikiwa kanisa. # Maelezo ya Jumla "ninyi" na "yenu" katika barua hii yanaonyesha wingi # Maelezo ya Jumla katika barua hii Yohana anatumia maneno "sisi" na 'yetu" ikimaanisha Yohana mwenyewe pamoja na wasomaji wake # Kutoka kwa mzee kwenda kwa mwanamke mteule na watoto wake Barua za wakati huo zilianza na jina la mwandishi, kwa kushupisha inaweza kusomeka:- " mimi, Yohana mzee, ninaandika barua hii kwa mwanamke mteule na watoto wake" # Mzee Ni rejea kwa Yohana, mtume na mwanafunzi wa Yesu. Anajiita mzee labda kwa sababu ya umri wake mkubwa au kwa sababu ni kiongozi kanisani. # kwa mwanamke mteule na watoto wake Pengine hii ina maana ya kundi au kusanyiko na waumini . # ambaye nampenda katika kweli. " Ninyi watu ninaowapenda katika kweli" # wanao ifahamu kweli "ambao wanao fahamu ukweli kuhusu Mungu na Yesu" # Baba...Mwana Hivi ni vyeo muhimu vinavyoelezea uhusiano kati ya Mungu na Yesu # katika kweli na upendo. Neno "kweli" linaelezea "upendo." Pengine inamaanisha "katika upendo wa kweli"