sw_tn/2co/11/07.md

24 lines
814 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Je, nilifanya dhambi kwa kujinyenyekeza mwenyewe ili ninyi muweze kuinuliwa
Paulo anaanza kwa kudai kwamba aliwatendea Wakorintho kwa uzuri.Swali hili la kujihoji linaweza kutafsiriwa hivi: " Nadhani tunakubaliana kwamba sikufanya dhambi kwa akujinyenyekeza mwenyewe ili ya kwamba mpate kuinuliwa"
# kwa uhuru
"bila kutegemea kurudishiwa chochote kutoka kwenu"
# Nilinyang'anya makanisa mengine
Sentensi hii imeelezwa kwa kuikuza au kutia chumvi kusisitiza kwamba Paulo alichukua fedha kutoka makanisa mengine.
# ningeweza kuwahudumia ninyi
Maaana kamili ya sentensi hii yaweza kuwa: "Naweza kuwatumikia ninyi bila gharama"
# Katika kila kitu nimejizuia mwenyewe kutokuwa mzigo kwenu
"sijawahi kwa njia yoyote kuwa mzigo kwenu kifedha.
# ndugu waliokuja
"Ndugu hawa" huenda walikuwa wanaume wote.