# Je, nilifanya dhambi kwa kujinyenyekeza mwenyewe ili ninyi muweze kuinuliwa Paulo anaanza kwa kudai kwamba aliwatendea Wakorintho kwa uzuri.Swali hili la kujihoji linaweza kutafsiriwa hivi: " Nadhani tunakubaliana kwamba sikufanya dhambi kwa akujinyenyekeza mwenyewe ili ya kwamba mpate kuinuliwa" # kwa uhuru "bila kutegemea kurudishiwa chochote kutoka kwenu" # Nilinyang'anya makanisa mengine Sentensi hii imeelezwa kwa kuikuza au kutia chumvi kusisitiza kwamba Paulo alichukua fedha kutoka makanisa mengine. # ningeweza kuwahudumia ninyi Maaana kamili ya sentensi hii yaweza kuwa: "Naweza kuwatumikia ninyi bila gharama" # Katika kila kitu nimejizuia mwenyewe kutokuwa mzigo kwenu "sijawahi kwa njia yoyote kuwa mzigo kwenu kifedha. # ndugu waliokuja "Ndugu hawa" huenda walikuwa wanaume wote.