sw_tn/1jn/03/16.md

32 lines
1013 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Kristo aliutoa uhai wake kwa ajili yetu.
Maelezo haya humaanisha: "Kristo kwa kupenda kwake mwenyewe aliutoa uhai wake kwa ajili yetu" au "Kristo kwa kupenda kwake alitufia sisi."
# Mali za ulimwengu.
"Mali zinazomilikiwa kama vile pesa, chakula, au nguo."
# Humuona ndugu yake mwenye uhitaji.
"Na humtambua muumini mwenzake anayehitaji msaada."
# Na huufunga moyo wake wa huruma kwa ajili yake.
Maelezo haya humaanisha kwamba, "lakini hamwonei huruma." au lakini hapendi kumsaidia."
# Upendo wa Mungu unakaaje ndani ya mtu huyo?
Yohana anatumia swali kuwafundisha wasikilizaji wake. Hii ingeweza kutafsiriwa kama usemi: "Upendo wa Mungu haumo ndani yake."
# Watoto wangu wapendwa.
"Watoto au wapendwa waumini wenzi wangu."
# Haya tusipende kwa maneno wala kwa mdomo.
Kifungu hiki, "kwa maneno" na "kwa mdomo" yote mawili yanalenga kile ambacho mtu anasema. " Usiseme tu ili mradi kwamba unawapenda watu."
# Bali katika matendo na kweli
"Bali onesha kwamba kweli unawapenda watu kwa kuwasaidia."