# Kristo aliutoa uhai wake kwa ajili yetu. Maelezo haya humaanisha: "Kristo kwa kupenda kwake mwenyewe aliutoa uhai wake kwa ajili yetu" au "Kristo kwa kupenda kwake alitufia sisi." # Mali za ulimwengu. "Mali zinazomilikiwa kama vile pesa, chakula, au nguo." # Humuona ndugu yake mwenye uhitaji. "Na humtambua muumini mwenzake anayehitaji msaada." # Na huufunga moyo wake wa huruma kwa ajili yake. Maelezo haya humaanisha kwamba, "lakini hamwonei huruma." au lakini hapendi kumsaidia." # Upendo wa Mungu unakaaje ndani ya mtu huyo? Yohana anatumia swali kuwafundisha wasikilizaji wake. Hii ingeweza kutafsiriwa kama usemi: "Upendo wa Mungu haumo ndani yake." # Watoto wangu wapendwa. "Watoto au wapendwa waumini wenzi wangu." # Haya tusipende kwa maneno wala kwa mdomo. Kifungu hiki, "kwa maneno" na "kwa mdomo" yote mawili yanalenga kile ambacho mtu anasema. " Usiseme tu ili mradi kwamba unawapenda watu." # Bali katika matendo na kweli "Bali onesha kwamba kweli unawapenda watu kwa kuwasaidia."