sw_tn/deu/23/21.md

32 lines
976 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli kana kwamba walikuwa mtu mmoja, kwa hiyo maneno "kwako" na "wako" hapa ni katika umoja.
# haupaswi kukawia kuikamilisha
"hautakiwi kutumia muda mrefu kukamilisha kiapo hiki"
# maana Yahwe Mungu wako hakika atadai kiapo hicho
"kwa sababu Yahwe Mungu wako atakulaumu na kukuadhibu iwapo hautakamilisha kiapo chako"
# Lakini iwapo utajizuia kutoa kiapo, haitakuwa dhambi kwako
Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Lakini, kama hautatoa kiapo, hautakuwa umetenda dhambi kwa sababu hautakuwa na kiapo cha kutimiza"
# Kile ambacho kimetoka kinywani mwako
Hii ni lahaja. "Maneno uliyozungumza"
# kulingana na kiapo ulichotamka kwa Yahwe Mungu wako
"chochote ulichoapa kwa Yahwe Mungu wako ambacho utafanya"
# chochote ulichotamka kwa hiari kwa kinywa chako
"chochote ambacho watu wamesikia ukiahidi kufanya kwa sababu ulitaka kukifanya"
# kinywa chako
"ili kwamba watu wasikie ukikitamka"