# Taarifa ya Jumla: Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli kana kwamba walikuwa mtu mmoja, kwa hiyo maneno "kwako" na "wako" hapa ni katika umoja. # haupaswi kukawia kuikamilisha "hautakiwi kutumia muda mrefu kukamilisha kiapo hiki" # maana Yahwe Mungu wako hakika atadai kiapo hicho "kwa sababu Yahwe Mungu wako atakulaumu na kukuadhibu iwapo hautakamilisha kiapo chako" # Lakini iwapo utajizuia kutoa kiapo, haitakuwa dhambi kwako Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Lakini, kama hautatoa kiapo, hautakuwa umetenda dhambi kwa sababu hautakuwa na kiapo cha kutimiza" # Kile ambacho kimetoka kinywani mwako Hii ni lahaja. "Maneno uliyozungumza" # kulingana na kiapo ulichotamka kwa Yahwe Mungu wako "chochote ulichoapa kwa Yahwe Mungu wako ambacho utafanya" # chochote ulichotamka kwa hiari kwa kinywa chako "chochote ambacho watu wamesikia ukiahidi kufanya kwa sababu ulitaka kukifanya" # kinywa chako "ili kwamba watu wasikie ukikitamka"