sw_ulb/58-PHM.usfm

44 lines
2.7 KiB
Plaintext

\id PHM
\ide UTF-8
\h Filemoni
\toc1 Filemoni
\toc2 Filemoni
\toc3 phm
\mt Filemoni
\c 1
\cl Sura 1
\p
\v 1 Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, na ndugu Timotheo kwa Filemoni, mpendwa rafiki yetu na mtenda kazi pamoja nasi,
\v 2 na kwa Afia dada yetu, na kwa Arkipas askari mwenzetu, na kwa kanisa lile linalokutana nyumbani kwako.
\v 3 Neema iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.
\p
\v 4 Wakati wote namshukuru Mungu wangu, ninakutaja katika maombi yangu,
\v 5 Kwa sababu nasikia kuhusu imani uliyonayo katika Bwana Yesu na upendo ulio nao kwa watakatifu wote.
\v 6 Ninaomba kwamba ushirika wa imani yenu iwe na ufanisi katika ujuzi wa kila jambo jema lililoko kati yetu katika Kristo.
\v 7 Kwa kuwa nimekuwa na furaha na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa sababu mioyo ya watakatifu wote imekuwa ikitulizwa nawe.
\p
\v 8 Kwa hiyo, ingawa nina ujasiri wote katika Kristo kukuamuru wewe kufanya kile unachoweza kufanya,
\v 9 lakini kwa sababu ya upendo, badala yake nakusihi - mimi, Paulo niliye mzee, na sasa ni mfungwa kwa ajili ya Kristo Yesu.
\v 10 Ninakusihi kuhusu mwanangu Onesmo, niliyemzaa katika vifungo vyangu.
\v 11 Kwa kuwa mwanzoni hakukufaa, lakini sasa anatufaa sote, wewe na mimi.
\p
\v 12 Mimi nimemtuma akurudie wewe, aliye moyo wangu hasa.
\v 13 Nataraji angeendelea kubaki pamoja nami, ili anitumikie badala yako, wakati niko kifungoni kwa ajili ya injili.
\v 14 Lakini sikutaka kufanya jambo lolote bila ruhusa yako. Nilifanya hivi ili kwamba jambo lolote zuri lisifanyike kwa sababu nilikulazimisha, bali kwa sababu ulipenda mwenyewe kulitenda.
\v 15 Labda ni sababu alitengwa nawe kwa muda, ilikuwa hivyo ili uwe pamoja naye milele.
\v 16 Ili kwamba asiwe tena mtumwa, bali bora zaidi ya mtumwa, kama ndugu mpendwa. Yeye ni mpendwa hasa kwangu, na zaidi sana kwako, katika mwili na katika Bwana.
\p
\v 17 Na hivyo kama wanichukulia mimi mshirika, mpokee kama ambavyo ungenipokea mimi.
\v 18 Lakini kama amekukosea jambo lolote, au unamdai kitu chochote, kidai hicho kutoka kwangu.
\v 19 Mimi Paulo, ninaandika kwa mkono wangu mwenyewe. Mimi nitakulipa pasipo na kukuambia yakua ninakudai wewe binafsi uhai hasa.
\p
\v 20 Naamu ndugu, acha nipate faida kutoka kwako katika Bwana; uiburudishe nafsi wangu katika Kristo.
\p
\v 21 Nikiwa na imani kuhusu utii wako, nakuandikia nikijua kwamba utafanya hata zaidi ya vile ninavyokuomba.
\p
\v 22 Wakati huo huo, andaa chumba cha wageni kwa ajili yangu, kwa kuwa ninatumaini kupitia maombi yako nitarudishwa kwenu.
\p
\v 23 Epafra, mfungwa mwenzangu katika Kristo Yesu anakusalimu,
\v 24 na kama afanyavyo Marko, Aristarko, Dema, Luka, watendakazi pamoja nami.
\v 25 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja na roho yako. Amina.