sw_tn/col/02/intro.md

1.1 KiB

Wakolosai 02 Maelezo kwa ujumla

Maswala muhimu katika sura hii

Tohara na ubatizo

Katika mistari ya 11-12, Paulo anatumia alama ya tohara ya agano la kale pamoja na alama ya ubatizo ya agano jipya kuchora taswira ya jinsi Wakristo wameungana na Kristo na kuokolewa kutoka kwa dhambi,

ehemu zingine zenye utata katika tafsiri ya sura hii"

Nyama

Hili ni swala ngumu. Labda "nyama" inatumiwa kama mfano ya asili yetu ya dhambi. Paulo hasemi kwamba mwili wa binadamu una dhambi. Ni kama Paulo anajaribu kusema kwamba wakati Wakiristo wanaishi ("katika nyama"), tutaendelea kutenda dhambi. Lakini asili yetu mpya itakuwa inapigana na asili yetu ya kale. Paulo anatumia pia "nyama" katika sura hii kumaanisha mwili wa binadamu.

Maana iliyosemwa

Paulo amevitaja vitu vingi katika sura hii kuashiria mambo yaliyokuwa yanalikumba kanisa la Wakolosai. Ni vyema kuacha maandiko yabaki bila kuelezea kwa uwazi kuhusu maswala yenyewe ya ukweli, (Tazama: rc://*/ta/man/translate/figs-explicit)

<< | >>