sw_tn/col/01/intro.md

33 lines
1.4 KiB
Markdown

# Wakolosai 01 Maelezo kwa ujumla
## Muundo na Mpangilio
Kama barua ya kawaida, Paulo ananza barua yake katika mistari ya 1-2 kwa kumtambulisha Timotheo na kujitambulisha kwa Wakristo wa Kolosai.
Paulo anazungumzia maswala mawili katika sura hii: Kristo ni nani na amefanyia Wakristo nini.
## Dhana maalum katika sura hii
### Ukweli wa siri
Paulo anaashiria ukweli wa siri katika sura hii. Jukumu la kanisa katika mipango ya Mungu halikujulikana hapo mwanzo. Lakini sasa Mungu amelitambulisha. Moja ya siri hii inahusisha watu wa Mataifa kuwa na nafasi sawa na Wayahudi katika mipango ya Mungu. (Tazama: [[rc://*/tw/dict/bible/kt/reveal]]).
## Mifano muhimu katika sura hii
### Picha za maisha ya Kikristo
Paulo anatumia picha nyingi kuelezea maisha ya Kikristo katika sura hii. Anatumia mifano ya "kutembea" na "Kuzaa matunda." (Tazama: [[rc://*/tw/dict/bible/other/fruit]]
## Sehemu zingine zenye utata katika tafsiri ya sura hii
### Kitendawili
Kitendawili ni kauli ya ukweli inayaonekana kuelezea kitu kisichowezekana. Mstari wa 24 ni kitandawili: "Sasa ninafurahia katika mateso yangu kwa ajili yenu." Mara nyingi watu hawafurahi wakati wanapoteseka. Lakini katika mistari ya 25-29 Paulo anaelezea ni kwa nini mateso yake ni mazuri. (Wakolosai 1:24)
## Links:
* __[Colossians 01:01 Notes](./01.md)__
* __[Colossians intro](../front/intro.md)__
__| [>>](../02/intro.md)__