sw_tn/psa/061/001.md

40 lines
1001 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.
# Taarifa ya Jumla:
Huu ni wimbo kuhusu uaminifu wa Mungu.
# Kwa mwanamuziki mkuu
"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"
# kwenye vyombo vya nyuzi
"watu wanapaswa kucheza vyombo vya nyuzi na wimbo huu"
# Zaburi ya Daudi
Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.
# Sikia kulia kwangu; jali ombi langu
Vishazi hivi viwili vinamaana sawa. "Mungu, nisikilize na ujibu ombi langu"
# umezidiwa
"umeshindwa"
# niongoze kwenye jiwe lililo juu zaidi yangu
Hapa mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni mwamba mkubwa anaoweza kupanda kwa ajili ya ulinzi.
# mnara imara kutoka kwa adui
Maneno yanayodokezwa "unaonilinda" yanaweza kuongezwa. "umekuwa kama mwamba imara unaonilinda dhidi ya adui wangu"
# mnara imara
Hapa mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni "mnara imara" unaotoa ulinzi dhidi ya adui zake.