# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # Taarifa ya Jumla: Huu ni wimbo kuhusu uaminifu wa Mungu. # Kwa mwanamuziki mkuu "Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu" # kwenye vyombo vya nyuzi "watu wanapaswa kucheza vyombo vya nyuzi na wimbo huu" # Zaburi ya Daudi Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi. # Sikia kulia kwangu; jali ombi langu Vishazi hivi viwili vinamaana sawa. "Mungu, nisikilize na ujibu ombi langu" # umezidiwa "umeshindwa" # niongoze kwenye jiwe lililo juu zaidi yangu Hapa mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni mwamba mkubwa anaoweza kupanda kwa ajili ya ulinzi. # mnara imara kutoka kwa adui Maneno yanayodokezwa "unaonilinda" yanaweza kuongezwa. "umekuwa kama mwamba imara unaonilinda dhidi ya adui wangu" # mnara imara Hapa mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni "mnara imara" unaotoa ulinzi dhidi ya adui zake.