sw_tn/psa/055/004.md

16 lines
695 B
Markdown

# Moyo wangu unatetemeka ndani yangu
Hapa, "moyo unatetemeka" inamaansiha maumivu yake ya kihisia au kuteseka. Kuteseka huku ni kwa sababu ya uoga. "Ninateseka kwa sababu ninaogopa sana"
# hofu yangu ya mauti imeniangukia
Kuwa na hofu sana inazungumziwa kana kwamba hofu ni kitu kinachomwangukia mtu. "Ninaogopa sana kuwa nitakufa" au "Ninahofu kuwa nitakufa"
# Uoga na kutetemeka zimeniangukia
Kuwa na hofu na kutetemeka kunazungumziwa kana kwamba hofu na kutetemeka ni vitu vinavyokuja kwa mtu. "Nimekuwa na hofu sana na kutetemeka"
# kitisho kimenilemea
Kuhisi kitisho inazungumziwa kana kwamba kitisho ni kitu kinachoweza kuwafunika watu. "Ninahisi kitisho kibaya" au "Ninahofu sana"