# Moyo wangu unatetemeka ndani yangu Hapa, "moyo unatetemeka" inamaansiha maumivu yake ya kihisia au kuteseka. Kuteseka huku ni kwa sababu ya uoga. "Ninateseka kwa sababu ninaogopa sana" # hofu yangu ya mauti imeniangukia Kuwa na hofu sana inazungumziwa kana kwamba hofu ni kitu kinachomwangukia mtu. "Ninaogopa sana kuwa nitakufa" au "Ninahofu kuwa nitakufa" # Uoga na kutetemeka zimeniangukia Kuwa na hofu na kutetemeka kunazungumziwa kana kwamba hofu na kutetemeka ni vitu vinavyokuja kwa mtu. "Nimekuwa na hofu sana na kutetemeka" # kitisho kimenilemea Kuhisi kitisho inazungumziwa kana kwamba kitisho ni kitu kinachoweza kuwafunika watu. "Ninahisi kitisho kibaya" au "Ninahofu sana"