sw_tn/psa/050/001.md

32 lines
932 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.
# Taarifa ya Jumla:
Zaburi hii ni wimbo unaofundisha watu.
# Zaburi ya Asafu
"Hii ni zaburi ambayo Asafu aliandika."
# Mwenye nguvu, Mungu, Yahwe
Mwandishi anatumia majina matatu tofauti kumzungumzia Mungu.
# akaiita dunia
Hapa neno "dunia" inamaanisha watu ambao wanaishi duniani. "akawaita watu wote"
# kutoka kuchomoza kwa jua hadi kuzama kwake
Msemo huu unamaanisha upande wa mashariki, ambapo jua huchomoza, na magharibi, ambapo jua huzama. Mwandishi anatumia tofauti hizi mbili kuwakilisha sehemu zote duniani. "kila sehemu duniani"
# Sayuni, ukamilisho wa uzuri
Maana zinazowezekana 1) "Sayuni, ambayo uzuri wake ni kamili" au 2) "Sayuni, mji mzuri zaidi."
# Mungu ameng'aa
Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni nuru inayong'aa. Hii inamaanisha Mungu kusababisha watu kujua kuhusu utukufu wake. "Utukufu wa Mungu unang'aa kama taa"