forked from WA-Catalog/sw_tn
20 lines
945 B
Markdown
20 lines
945 B
Markdown
# Akabariki nafsi yake
|
|
|
|
Hapa neno "nafsi" linamaanisha mtu mzima. Msemo huu unamaanisha kuwa alijiona kuwa na furaha na mafanikio kwa sababu ya utajiri wake. "Akajipongeza mwenyewe"
|
|
|
|
# na watu wanakusifu unapoishi kwa ajili yako mwenyewe
|
|
|
|
Hapa mwandishi anatoa kauli ya ujumla kuhusu jinsi watu wanavyozungumza kuhusu watu wengine waliofanikiwa kulingana na mtazamo wa kidunia.
|
|
|
|
# unapoishi kwa ajili yako mwenyewe
|
|
|
|
Msemo huu unamaanisha kuishi kwa mafanikio kulingana na mtazamo wa kidunia. "fanya vyema kwa ajili yako" au "ishi kwa mafanikio"
|
|
|
|
# ataenda katika kizazi cha baba zake
|
|
|
|
"ataenda mahali kizazi cha baba yake kilipo." Hii ni tasifida inayomaanisha kwamba mtu tajiri atakufa na kuungana na mababu zake kaburini. "ataungana na mababu zake kaburini"
|
|
|
|
# hawataona nuru tena
|
|
|
|
wale ambao "hawataona" ni mtu tajiri na mababu zake. Neno "nuru" inaweza kuwa inamaanisha jua au ni sitiari ya uhai. "hawataliona jua tena" au "hawataishi tena"
|