sw_tn/rev/13/03.md

33 lines
826 B
Markdown

# Lakini jeraha lake likapona
"Lakini hilo jeraha lilipona"
# jeraha la kusababisha mauti
"jeraha baya." Hili ni jeraha kubwa linaloweza kusababisha mtu kufa.
# dunia yote
Neno "dunia" inamaanisha watu waliomo ndani yake. "watu wote duniani"
# ikamfuata mnyama
"ikamtii mnyama"
# joka
Hili lilikuwa tambaazi kubwa kali, kama mjusi. Kwa wayahudi ilikuwa ni alama ya uovu na machafuko. Joka linatambulika pia katika mstari wa 9 kama "ibilisi au Shetani"
# alimpa mamlaka yule mnyama
"alimfanya mnyama kuwa na mamlaka kama aliyokuwa nayo yeye"
# Nani kama mnyama?
Hili swali linaonesha ni jinsi gani walivyostaajabishwa na mnyama. "Hakuna aliye na nguvu kama mnyama!"
# Nani atapigana naye?
Hiil swali linaonesha kiasi gani watu walihofia nguvu ya mnyama. "Hakuna mtu atakayeweza kupigana na mnyama na kushinda!"