sw_tn/psa/018/046.md

21 lines
655 B
Markdown

# na mwamba wangu usifiwe
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "yeye ni mwamba wangu na anapaswa kusifiwa" au "watu wasifu mwamba wangu"
# mwamba wangu
Hapa mwandishi anazungumzia ulinzi wa Yahwe kana kwamba alikuwa ni mwamba uliozuia adui zake kumfikia.
# Na Mungu wa wokovu wangu ainuliwe
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Na watu wamtukuze Mungu wa wokovu wangu"
# Mungu wa wokovu wangu
Hii inamaanisha kuwa Mungu amemuokoa. "Mungu aliyeniokoa"
# Mungu anayetekeleza kisasi kwa ajili yangu
"Kutekeleza kisasi" inamaana kuwaadhibu watu kwa matendo yao maovu. "Mungu anayewaadhibu watu kwa matendo maovu waliyotenda kwangu"