# na mwamba wangu usifiwe Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "yeye ni mwamba wangu na anapaswa kusifiwa" au "watu wasifu mwamba wangu" # mwamba wangu Hapa mwandishi anazungumzia ulinzi wa Yahwe kana kwamba alikuwa ni mwamba uliozuia adui zake kumfikia. # Na Mungu wa wokovu wangu ainuliwe Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Na watu wamtukuze Mungu wa wokovu wangu" # Mungu wa wokovu wangu Hii inamaanisha kuwa Mungu amemuokoa. "Mungu aliyeniokoa" # Mungu anayetekeleza kisasi kwa ajili yangu "Kutekeleza kisasi" inamaana kuwaadhibu watu kwa matendo yao maovu. "Mungu anayewaadhibu watu kwa matendo maovu waliyotenda kwangu"