sw_tn/psa/005/009.md

41 lines
1.0 KiB
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Daudi anawazungumzia adui zake
# Kwa kuwa hakuna ukweli midomoni mwao
Ukweli kuwa midomoni mwao inamaanisha kuongea ukweli. "Kwa kuwa huwa hawasemi ya kweli"
# utu wao wa ndani ni uovu
Utu wao wa ndani inamaanisha mawazo ya watu na tamaa zao. "mawazo yao na tamaa ni mbaya"
# koo yao
Koo inaashiria maneno ya watu. "maneno yao" au "kile wanchosema"
# koo yao ni kaburi lililo wazi
Koo yao inazungumziwa kana kwamba ni kaburi lililo wazi, tayari kwa ajili ya maiti kuwekwamo. Maana zinazowezekana ni 1) "wanasema watawaua watu" au 2) "Wanachosema huua watu"
# wanijipendekeza na ulimi wao
"wanasema vitu vizuri kuhusu watu wengine bila kumaanisha"
# ulimi wao
Ulimi unaashiria kile wanachosema watu.
# njama zao ziwe anguko lao
"njama zao ziwasababishe kupitia maafa" au "wapunguze umuhimu wao kwa sababu ya njama zao"
# njama
mipango ya kuwadhuru watu
# anguko
Hili ni jambo linalowafanya watu kupitia maafa na kupoteza nguvu. Kupitia maafa au kupoteza umuhimu inazungumziwa kama kuangaku.