sw_tn/jos/22/24.md

551 B

Maelezo ya jumla

Makabila ya Rubeni, Gadi na nusu ya Manase wanatoa majibu yao sasa.

watoto wenu wanaweza kuwaambia watoto wetu.....Mungu wa Israeli?

Haya ni mashitaka ya kinadharia ambayo makabila haya matatu yanadhani kuwa watoto wa makabila mengine wangeweza kufanya kwa wakati ujao.

Mna nini ninyi na Yahweh, Mungu wa Israeli?

Makabila matatu yanatumia swali lisilohitaji majibu ili kutilia mkazo juu ya hali ambayo walikuwa wakiiepuka. Swali hili laweza kuandikwa kama maelezo. "Hamna kitu cha kufanya na Yahweh, Mungu wa Israeli."