sw_tn/dan/04/36.md

1.1 KiB

Maelezo ya jumla

Katika mistari ya 34-37 Nebukadneza anaongelea katika nafsi ya kwanza katika kueleza jibu lake kwa Mungu.

utimamu wa akili zangu uliponirudia

Mahali hapa utimamu unaongelewa kana kwamba ulikuwa na uwezo wa kurudi kwa nguvu zake.

utukufu wangu na fahari yangu ilinirudia

Mahali hapa utukufu wake na fahari kwa pamoja unaongelewa kana kwamba ulikuwa na uwezo wa kurudi kwa nguvu zake .

utukufu wangu na fahari yangu

Maneno haya yana maana sawa na yametumika kutilia mkazo juu ya ukubwa wa utukufu wake.

watu wenye heshima walitafuta msaada wangu

"Watu wangu wa heshima waliomba msaada wangu tena"

Nilirudishwa kwenye kiti changu cha enzi, na nilipewa ukuu zaidi

Mahali hapamaneno "kiti cha enzi" yanarejelea mamlaka yake ya kutawala. Pia muundo tendaji waweza kutumika. "Nilirudi kutawala ufalme wangu tena, na nilipata ukubwa zaidi."

ninamsifu, ninamtukuza na kumheshimu

Maneno haya matatu kimsingi yana maana moja na yametumika kutia mkazo juu ya jinsi alivyomsifu Mungu.

wanaotembea katika kiburi chao wenyewe.

Kitenzi "kutembea" kinamrejelea mtu anayetenda kwa kiburi.