sw_tn/act/05/09.md

21 lines
537 B
Markdown

# Sentensi unganishi:
Huu ni mwisho wa sehemu ya habari kuhusu Anania na Safira.
# Inakuwaje kwamba mmepatana kwa pamoja kumjaribu Roho wa Bwana?
Petro aliuliza hili kuonyesha hawa wawili kwamba walikubaliana kutenda dhambi kwa pamoja. "Mmekubaliana kwa pamoja kumjaribu Roho!"
# miguu ya wale waliomzika mme wako
Hapa "Miguu" inamaanisha wanaume waliomzika Anania.
# akadondoka miguuni pa Petro
Inamaanisha Safira alipokufa alidondoka mbele yamiguu ya Petro
# Akapumua pumzi ya mwisho
Hii ni namna ya kusema kwamba "alikufa."