sw_tn/act/04/intro.md

1.6 KiB

Matendo 04 Maelezo kwa jumla

Muundo na Mpangilio

Tafsiri zingine zimetenga kila mstari wa ushairi kulia zaidi kuliko maandishi mengine ili isomeke vyema.ULB hufanya hivi na ushairi ulionukuliwa kutoka Agano la kale 4:25-26

DHANA MAALUM KATIKA SURA HII

umoja

Wakristo wa kwanza walitamani sana kuwa na umoja, Walitaka kuamini mambo sawa na kusaidiana kwa kila kitu walichokimiliki huku wakisaidia pia waliohitaji.

"Ishara na Maajabu"

Maneno haya yanaashiria vitu ambavyo vinaeza kufanywa tu na Mungu. Wakristo walitaka Mungu afanye yale tu ambayo angeweza kuyafanya ili watu waamini kwamba waliyoyanena kumhusu Yesu yalikuwa ya ukweli.

Mifano muhimu kwenye hii sura

Jiwe la pembeni

Jiwe la pembeni lilikuwa kipande cha jiwe kilichowekwa chini wakati wa ujenzi wa jengo. Neno hili limetumika kumaanisha sehemu muhimu ya kitu,ile sehemu tegemeo. Kusema ya kwamba Yesu ni jiwe kuu la pembeni la kanisa ni kusema kwamba hakuna kitu ndani ya kanisa kilicho na umuhimu kuliko Yesu na ya kwamba kila kitu ndani ya kanisa kinamtegemea, (Tazama: rc://en/ta/man/translate/figs-metaphor and rc://en/tw/dict/bible/kt/faith)

Sehemu zingine zenye utata katika tafsiri ya sura hii.

Jina

"Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo" (Matendo 4:12). Kwa maneno haya Petro alimaanisha kwamba hamna mtu yeyote ambaye amewahi kuwa duniani ama atakayekuja duniani kuwaokoa watu.

<< | >>