sw_tn/act/04/01.md

33 lines
1015 B
Markdown

# Sentensi unganishi
Viongozi wa dini walimkamata Petro na Yohana baada ya Petro kumponya yule mtu aliyezaliwa kiwete.
# wakaja kwao
"waliwasogelea" au "walikuja kwao"
# Walikuwa wameudhika sana
Walikuwa na hasira. Masadukayo kwa upekee wao wangekuwa na hasira kwa Petro na Yohana kwasababu hawakuamini ufufuo.
# walikuwa wanawafundisha watu kuhusu Yesu na kutangaza juu ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu
Petro na Yohana walikuwa wakisema Mungu angewainua watu kutoka mautini sawa na vile Yesu alivyoinuliwa kutoka miongoni mwa wafu. Petro anazungumzia ufufuo wa Yesu na ufufuo wa watu wote kwa ujumla.
# Waliwakamata
Makuhani na mlinzi wa hekalu pamoja na Masadukayo waliwakamata Petro na Yohana.
# Kwavile ilikuwa jioni sasa
Ilikuwa tendo la kawaida kutowahoji watu wakati wa usiku.
# na idadi ya wanaume waliokuwa wameamini
Hii inamanisha kwa idadi ya wanaume tu, wanawake na watoto walioamini hawakuhesabiwa.
# Walikuwa yapata elfu tano
"walikuwa kama elfu tano" au "iliongezeka hadi elfu tano"