sw_tn/act/01/intro.md

2.5 KiB

Matendo 01 Maelezo ya Jumla

Muundo na mpangilio

Sura hii inarekodi tukio,kawaida linajulikana kama "kupaa", wakati Yesu alirudi mbinguni baada ya ufufuko wake. Hatarudi tena mpaka "Ujio wake wa pili." (rejelea: rc://en/tw/dict/bible/kt/heaven and rc://en/tw/dict/bible/kt/resurrection).

Toleo la UDB limeweka maneno "Kwa mpendwa Theofila" kando na maneno mengine. Hii ni kwa sabau Waiingereza huanza kuandika barua namna hivi. Unaeza anza kitabu hiki jinzi watu huanza kuandika waraka katika mila yako.

Tafsiri zingine zinanukuu kutoka Agano la Kale kwenye kulia kwa ukurasa kuliko maandiko yote kwa jumla. ULB hufanya hivi kupitia nukuu mbili kutoka Zaburi 1:20

DHANA MAALUM KATIKA SURA HII

BATIZA

Neno "batiza" lina maana mbili katika sura huu. Inaashiria ubatizo wa Yohana na ubatizo wa Roho Mtakatifu (Matendo 1:5). (Tazama: : rc://en/tw/dict/bible/kt/baptize)

"Alizungumza kuhusu ufalme wa Mungu"

Wasomi wengine huamini kuwa wakati Yesu "alipozungumzuia kuhusu ufalme wa Mungu," aliwaeleza wanafunzi wake ni kwa nini ufalme wa Mungu haukuja kabla ya kifo chake. Wengine huamini kwamba ufalme wa Mungu ulianza wakati Yesu alikuwa hai na ya kwamba hapa Yesu alikuwa anafafanua kwamba huu ulikuwa mwanzo kwa umbo jipya.

Matatizo mengine ya tafsiri katika sura hii.

wanafunzi kumi na wawili

yafuatayo ni majina ya wanafunzi kumi na wawili

Katika Injili ya Matayo

Wa kwanza Simoni aliyeitwa Petro, na Andrea nduguye; Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye; Filipo, na Bartholomayo; Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo, na Thadayo;Simoni Mkananayo, na Yuda Iskariote

Katika injili ya Marko

Simoni (Petro),Andrea,na Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye Yakobo, akawapa jina la Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo; na Filipo, na Bartholomayo, na Mathayo, na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Thadayo, na Simoni Mkananayo, na Yuda Iskariote.

Katika injili ya Luka

Simoni(Petero),Andrea,Yakobo,Yohana,Filipo,Bartholomayo,Matayo,Tomaso,Yakobo wa Alfayo,Simoni Mkananayo,Yuda wa Yakobo na Yuda Iskariote.

Kuna uwezekano ya kwamba Thadayo na Yuda wa Yakobo ni mtu mmoja

Akeldama

Hili ni neno la Kihebrania au Kiaramaiki. Luka alitumia maneno ya Kigiriki ili wasomaji wake wajue lilivyotamkua,kisha akawaeleza maana yake. Unatakikana kulitamka jinsi linalatamkwa kwa lugha yako kisha ukaeleza maana yake.(Tazama: rc://en/ta/man/translate/translate-transliterate)

| >>