sw_tn/2co/03/01.md

1.6 KiB

Sentensi Unganishi

Paulo anawakumbusha kuwa hajisifu kwa vile anavyowaambia kuhusu kile alichokifanya kuhusu Kristo.

Tunaanza kujisifu wenyewe tena ?

" Hatujaanza kujisifu wenyewe tena"

hatuhitaji barua za utambulisho kwenu au kutoka kwenu, kama watu wengine, tunafanya hivyo?

"Kwa hakika hatuhitaji barua za uthibitisho kwenu au kutoka kwenu, kama watu wengine wanavyofanya"

Barua za uthibitisho

Hii ni barua mtu huandika kujitambulisha na kutoa uthibitisho wa mtu mwingine.

Ninyi wenyewe ni barua yetu ya utambulisho wetu

Ninyi wenyewe ni sawa na barua ya utambulisho wetu"

Imeandikwa ndani ya mioyoni mwetu

"ambayo Kristo ameiandika mioyoni mwetu"

imejulikana na kusomwa na watu wote

"ambayo watu wote wanaweza kuifahamu na kuisoma"

ninyi ni barua kutoka kwa Kristo

" ninyi ni barua ambayo Kristo ameiandika"

imetolewa na sisi

"ambayo tuliitoa"

Imeandikwa siyo kwa wino...katika vibao vya mioyo ya watu

Paulo anafafanua kwamba Wakorintho ni sawa na barua ya kiroho, siyo sawa na barua ambayo wanandamu huandika kwa vifaa vinavoonekana.

Imeandikwa si kwa wino...bali kwa roho wa Mungu anyeishi

"siyo barua ambayo watu huandika kwa wino, bali ni barua ambayo imeandikwa na Mungu anayeishi"

Haikuandikwa juu ya mbao za mawe, bali imeandikwa juu ya mbao za mioyo ya wanadamu

"siyo barua ambayo watu huchonga juu ya mbao za mawe bali ni barua ambayo Roho wa Mungu anayeishi ameiandika juu ya mbao za mioyo ya watu"

mbao za mioyo ya watu

Paulo anazungumza kuhusu mioyo yao ambayo imekuwa kama vipande bapa vya mawe au udongo wa mfinyanzi juu yake watu wamechora barua.