sw_tn/1pe/05/intro.md

1.4 KiB

1 Petero 05 Maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

Watu wengi wa kale katika Mashariki ya karibu wangemalizia barua jinsi Petero anavyoimalizia hii.

Dhana muhimu katika sura hii

Mataji

Taji ambalo mchungaji Mkuu atapeana ni tuzo, kitu ambacho watu hupokea wakitenda mema. (Tazama: //en/tw/dict/bible/other/reward)

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

Simba

Wanyama wote wanawaogopa simba kwa sababu ya kasi na nguvu zao na pia wanakula karibu kila aina za wanyama. Pia wanakula binadamu. Shetani anataka kuwafanya watu wa Mungu kuwa waoga na kwa hivyo Petero anatumia mfano ya simba kufundisha wasomaji wake kwamba Shetani anaweza kudhuru miili yao. Lakini wakimwamini Mungu na kumtii, watakuwa watu wa Mungu na Mungu atawahudumia, (Tazama: rc://en/ta/man/translate/figs-simile)

Babuloni

"Babuloni ilikuwa taifa ovu katika Agano la Kale. Taifa hilo liliharibu jiji la Yerusalemu na likawateka Wayahudi kutoka maboma yao na wakawatawala. Petero anatumia Babuloni kama mfano ya taifa ambalo lilikuwa linawatesa Wakristo aliokuwa anawaandikia. Huenda aliamaanisha Yerusalemu kwa sababu Wayahudi walikuwa wanawatesa sana Wakristo ama aliashiria Roma kwa sababu Warumi walikuwa wanawatesa Wakristo. (Tazama: rc://en/tw/dict/bible/kt/evil and rc://en/ta/man/translate/figs-metaphor)

__<< | __