sw_tn/1co/11/intro.md

34 lines
1.8 KiB
Markdown

# 1 Wakorintho 11 Maelezo ya Jumla
### Muundo na upangiliaji
Huu ni mwanzo wa sehemu mpya wa barua (Sura za 11-14). Paulo sasa anazungumza kuhusu huduma nzuri za kanisa. Katika sura hii, anahusisha matatizo mawili tofauti: wanawake katika huduma za kanisa (mistari ya 1-16) na Meza ya Bwana (mistari ya 17-34).
### Dhana maalum katika sura hii
#### Mazoezi mema katika huduma ya kanisa
#### Wanawake wasio na adabu
Maagizo ya Paulo hapa yanajadiliwa na wasomi. Labda kulikuwa wanawake ambao walikuwa wakitumia uhuru wao wa Kikristo vibaya a kuleta fujo ndani ya kanisa sababu hawakukuwa na adabu ya kawaida. Fujo kutokana na vitendo vyao vilimfanya awe na wasiwasi.
#### Meza ya Bwana
Kulikuwa na matatizo katika Wakorintho kwa jinsi walikula Meza ya Bwana. Hawakutenda kwa umoja. katika Wakorintho kwa jinsi walikula Meza ya Bwana, baadhi yao walikula chakula chao wenyewe bila kushirikiana. Baadhi yao walilewa wakati watu masikini walipokuwa na njaa. Paulo alifundisha kwamba waumini wanadharau kifo cha Kristo kama wanakula Meza ya Bwana na kufanya dhambi au wakati
wanavunja ushirika na wenzao. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/sin]] and [[rc://en/tw/dict/bible/kt/reconcile)
### Mifanyo ya muhimu za matamshi katika sura hii
#### Maswali ya uhuishaji
Paulo hutumia maswali ya uhuishaji ili kuwakaripia watu kwa kutofuata kwao sheria za ibada aliyopendekeza. (See: rc://en/ta/man/translate/figs-rquestion)
#### Kichwa
Paulo anatumia "kichwa" kama kielelezo cha mamlaka katika mstari wa 3 na pia kutaja kichwa halisi cha mtu katika mstari wa 4 na kuendelea. Kwa kuwa hayo ni ya karibu sana, inawezekana kwamba Paulo alitumia "kichwa" kwa makusudi kwa njia hii. Hii inaonyesha kwamba mawazo katika aya hizi ziliunganishwa. (See: rc://en/ta/man/translate/figs-metonymy)
## Links:
* __[1 Corinthians 11:01 Notes](./01.md)__
__[<<](../10/intro.md) | [>>](../12/intro.md)__