sw_tn/tit/02/intro.md

799 B

Tito 02 Maelezo kwa jumla

Dhana muhimu katika sura hii

Majukumu ya kijinsia

Wasomi wanatofautiana kuhusu jinsi ya kuielewa aya hii katika muktadha wake wa kihistoria na kitamaduni. Wasomi wengine wanaamini kwamba wanaume na wanawake wako sawa kwa maswala yote. Wengine wanaamini Mungu aliwaumba wanaume na wanawake kutumikia majukumu ya kipekee katika kanisa na ndoa.Watafsiri wawe makini wasiathiriwe na jinsi wanavyoelewa swala hili wakati wa kutafsiri aya hii.

Utumwa

Katika sura hii, Paulo haandiki iwapo utumwa ni mzuri ama mbaya. Paulo anafundisha kwamba watumwa wawafanyie mabwana wao kazi kwa uaminifu. Anawafundisha waumini wote kumcha Mungu na kuishi vyema katika kila hali.

<< | >>