sw_tn/sng/02/03.md

997 B

Kama mti wa mpera ... kijana mdogo

Kama mti wa mpera ni zaidi ya faraja na furaha zaidi ya miti yote msituni kwa hiyo mpendwa wa mwanamke ni zaidi ya faraja na furaha zaidi ya wanaume wadogo wote

Mti wa mpera

Mti unaozaa matunda madogo ya njano ambayo ni matamu sana

Nina kaa chini ya kivuli chake kwa furaha sana

Mwanamke anapata furaha na faraja akiwa karibu na mpendwa wake

Na tunda lake ni tamu kwa ladha yangu

Mwanamke analinganisha starehe anayo ipata kwa mpendwa wake na tunda tamu

Ukumbi wa maakuli

Ni chumba kikubwa ambapo watu hula mlo mkubwa na kufurahia kutembeleana

Na bendera yake

"bendera" ni kipande kikubwa cha nguo ambacho watu hupeperushwa juu mbele ya jeshi ili kuongoza na kuwapa ujasiri wanaume wengine

Bendera yake juu yangu ilikuwa upendo

Mwanamke angeweza kuwa na wasiwasi wa kuingia ukumbi wa maakuli, lakini mapenzi ya mpendwa wake yalimuonesha njia na kumpa ujasiri wa kuingia. "lakini upendo wake uliniongoza nakunipa ujasiri kama bendera."