# Kama mti wa mpera ... kijana mdogo Kama mti wa mpera ni zaidi ya faraja na furaha zaidi ya miti yote msituni kwa hiyo mpendwa wa mwanamke ni zaidi ya faraja na furaha zaidi ya wanaume wadogo wote # Mti wa mpera Mti unaozaa matunda madogo ya njano ambayo ni matamu sana # Nina kaa chini ya kivuli chake kwa furaha sana Mwanamke anapata furaha na faraja akiwa karibu na mpendwa wake # Na tunda lake ni tamu kwa ladha yangu Mwanamke analinganisha starehe anayo ipata kwa mpendwa wake na tunda tamu # Ukumbi wa maakuli Ni chumba kikubwa ambapo watu hula mlo mkubwa na kufurahia kutembeleana # Na bendera yake "bendera" ni kipande kikubwa cha nguo ambacho watu hupeperushwa juu mbele ya jeshi ili kuongoza na kuwapa ujasiri wanaume wengine # Bendera yake juu yangu ilikuwa upendo Mwanamke angeweza kuwa na wasiwasi wa kuingia ukumbi wa maakuli, lakini mapenzi ya mpendwa wake yalimuonesha njia na kumpa ujasiri wa kuingia. "lakini upendo wake uliniongoza nakunipa ujasiri kama bendera."