sw_tn/rom/08/intro.md

2.8 KiB

Warumi 08 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Mstari wa kwanza wa sura hii ni sentensi ya kupita. Paulo anahitimisha mafundisho yake ya Sura ya 7 na anaongoza katika ya maneno ya Sura ya 8.

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB inafanya hii kwa mstari wa 36. Paulo ananukuu maneno haya kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

Kuishi ndani kwa Roho

Roho Mtakatifu anasemekana kuishi ndani ya mtu au ndani ya moyo wao. Ikiwa Roho yupo, hii inaashiria kwamba mtu ameokolewa. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/save)

"Hawa ni wana wa Mungu"

Yesu ni Mwana wa Mungu kwa njia ya pekee. Mungu pia anachukua Wakristo kuwa watoto wake. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/sonofgod]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/adoption]])

Kuchaguliwa mapema

Wasomi wengi wanamwamini Paulo katika sura hii anafundisha sana juu ya somo inayojulikana kama "kuchaguliwa mapema." Hii inahusiana na dhana ya Biblia ya "kuchagua mapema." Wengine huchukua hii ili kuonyesha kwamba Mungu, tangu kabla ya msingi wa dunia, alichagua watu wengine kuokoa milele. Wakristo wana maoni tofauti juu ya kile Biblia inafundisha juu ya suala hili. Hivyo watafsiri wanahitaji kuchukua tahadhari ya ziada wakati wa kutafsiri sura hii, hasa kuhusiana na mambo ya kusababisha. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/predestine]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/save]])

Mifano muhimu ya matamshi katika sura hii

Mfano

Paulo anaeleza mafundisho yake kishairi katika mstari wa 38 na 39 kwa njia ya mfano iliyopanuliwa. Anaeleza kuwa hakuna chochote kinachoweza kumtenganisha mtu na upendo wa Mungu ndani ya Yesu. (See: rc://*/ta/man/translate/figs-metaphor)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Hakuna hukumu

Kifungu hiki kinapaswa kutafsiriwa kwa uangalifu ili kuepuka kuchanganyikiwa kwa mafundisho. Watu bado wana hatia ya dhambi zao. Mungu anakataa kutenda kwa dhambi, hata baada ya kumwamini Yesu. Mungu bado anaadhibu dhambi za waumini, lakini Yesu amelipa adhabu kwa dhambi zao. Hii ndio Paulo anavyoonyesha hapa. Neno "kulaani" ina maana nyingi. Hapa Paulo anasisitiza kwamba watu ambao wanamwamini Yesu hawaadhibiwi tena milele kwa ajili ya dhambi yao kwa "kuhukumiwa kuzimu." (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/guilt]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/faith]] and rc://*/tw/dict/bible/kt/condemn)

Mwili

Hii ni suala ngumu. "Mwili" ni mfano ya asili yetu ya dhambi. Paulo hafundishi kwamba miili yetu ya kimwili ni dhambi. Inaonekana kama Paulo anafundisha kwamba wakati wote Wakristo wanaishi ("katika mwili"), tutaendelea kutenda dhambi. Lakini asili yetu mpya itapigana dhidi ya asili yetu ya zamani. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/flesh)

<< | >>