sw_tn/rom/01/11.md

501 B

Sentensi unganishi:

Paulo anaendelea kuweka wazi maelezo yake kwa watu wa Rumi kwa kuelezea shauku yake ya kuwaona mmoja mmoja.

Kwa kuwa natamani kuwaona

"kwa kuwa nataka kuwaona"

Kwa kuwa

"kwa sababu"

baadhi ya zawadi za roho, ili kuwatia nguvu

"baadhi ya zawadi toka kwa Roho Mtakatifu, ambayo itawasaidia na kuwatia nguvu"

Ambayo ni, mfarijiane kati yenu, kupitia imani ya kila mtu, yenu na yangu

"Namaanisha kwamba nataka tutiane moyo kwa kutumia uzoefu wa imani yetu kwa Yesu"