sw_tn/rev/11/intro.md

2.0 KiB

Ufunuo 11 Maelezo ya jumla

Muundo na mpangilio

Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo msitari wa ushairi ili isomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi na ushairi ulioko katika 11:15, 17-18.

ole

Kuna aina nyingi maalum za "ole" ambazo zimetajwa katika kitabu cha Ufunuo.Sura hii ina ole ya pili na ya tatu. Labda ole hizi zina maana muhimu fulani kulingana na matukio ya kitabo cha Ufunuo.

Dhana muhimu katika sura hii

Watu wa mataifa

"Watu wa mataifa katika sura hii wanaashiria watu wa mataifa wasio mcha Mungu na sio watu wa mataifa ambao ni Wakristo. (Tazama: rc://*/tw/dict/bible/kt/ungodly)

Mashahidi wawili

Mashahidi hawa wawili wana umuhimu kama manabii wakati wa kipindi cha Ufunuo. Wasomi wamependekeza vitu vingi kuhusu utambulisho wa hawa wanaume wawili. Haijulikani na haina umuhimu wa kujua hawa walikuwa akina nani.Badalayake, ni asili yao isiyoangamika na ujumbe wao ambao ni muhimu na haikataliki. (Tazama: rc://*/tw/dict/bible/kt/prophet)

Shimo lisilo na mwisho

Hii ni taswira ya kawaida katika kitabu cha ufunuo kinachoashiria kuzimu. Inasisitiza kwamba kuzimu haiepukiki. Inaelezewa kama iliyoko chini lakini mbinguni inayoelezewa kama iliyo juu. (Tazama: rc://*/tw/dict/bible/kt/hell)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

"Hawa manabii wawili waliwatesa watu walioishi duniani"

Hawa manabii wawili wanahusishwa na uharbifu mkubwa utakaosababisha hasara kubwa kwa watu duniani. Hii siyo roho mbaya mbali ni jaribio la kuwaleta watu hawa kwa toba. Lakini hawatatubu. (Tazama: [[rc:///tw/dict/bible/kt/repent]] na [[rc:///ta/man/translate/figs-explicit]])

"Wakati umetimia wa wafu kuhukumiwa"

Watu watahukumiwa baada ya kufa.Wale wanaomkataa Yesu watapata mateso ya milele. Lakini Wakristo watatuzwa kwa uaminifu wao walioishi maisha yao kama Wakristo. (Tazama: [[rc:///tw/dict/bible/kt/eternity]] na [[rc:///tw/dict/bible/kt/faithful]])

<< | >>