sw_tn/rev/09/intro.md

2.9 KiB

funuo 09 Maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

Sura hii inaendeleza hukumu za baragumu saba. Hii sura na ile iliyopita inajumuisha kitengo kimoja.

Ole

Kuna aina nyingi za "ole" maalum ambazo zimetajwa katika kitabu cha Ufunuo. Sura hii ina ole hizi za kwanza. Kuna uwezekano hizi zina maana ya umuhimu wa kimuundo wa matukio kulingana na wakati katika Ufunuo.

Dhana muhimu katika sura hii

Picha ya mnyama

Mfano ya mnyama ni kawaida katika kitabu hiki na pia kwenye hii sura.Watu wa kale wa mashariki ya karibu huenda waliwatazama hawa wanyama kama wenye walikua na 'tabia fulani' iliyoakilisha wanyama hawa. Kwa mfano simba mara nyingi huonekana kama aliye na nguvu. Mtafsiri asijaribu kutoa maana ya kila picha hizi.

Shimo lisilo na mwisho

Hii ni mfano ya kawaida katika kitabu cha Ufunuo kinachoashiria kuzimu.Inasisitiza kwamba kuzima haiwezi kuepukwa. "Inaelezewa kama iliyoko chini kinyume na mbinguni inayoelezewa kama iliyo juu. Hii inasisitza kwamba hakuna mbinguni wala kuzimu hapa duniani. (Tazama: rc://*/tw/dict/bible/kt/hell)

Abadoni na Apolioni

"Abadoni" ni neno la Kiebrania na neno "Apolioni" ni neno la Kigiriki. Maneno yote yanamaanisha "Mwangamizi". Yohana alitafsiri Mwangamizi neno hilo la Kiebrania kwa kuiandika na herufi za Kigiriki.Watafsiri wa ULB na UDB waliyatafsiri kutumia herufi za Kingereza. Watafsiri wanashauriwa kutafsiri maneno haya kutumia herufi za lugha kusudiwa.Kwa vile wasomaji wa asili wa Wagiriki wangeelewa maana ya "Apoloni," watafsiri wanaweza kutoa maana yake katika maelezo ya tanbihi.

Toba

Sura hii inataja dhamira ya toba. Hata ingawa kuna miujiza mingi, watu wanasemekana kuepuka toba na kubaki dhambini. Si vizuri kusahau dhamira hii ukisoma kitabo cha Ufunuo. (Tazama: [[rc:///tw/dict/bible/kt/repent]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/sin]])

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii.

Mfano

Shetani mara nyingi anafanuliwa kama malaika aliyeanguka. Sababu nyota ni mfano wa malaika katika kitabu cha Ufunuo,maneno "nyota kutoka mbinguni iliyokuwa imeanguka" huenda inaashiria Shetani. (Tazama: [[rc:///tw/dict/bible/kt/satan]], [[rc:///ta/man/translate/writing-symlanguage]] na rc://*/ta/man/translate/writing-apocalypticwriting)

Kuna Kuna mifano nyingi katika sura hii. Kazi yao ni kuonyesha picha ngumu ambazo Yohana anaona katika maono yake.Kwa hivyo mifano hii inaangazia maswala yanayowezekana kuliko kuangazia kazi ya kishairi. (Tazama: rc://*/ta/man/translate/figs-simile)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

"Wale watu ambao hawakuwa na muhuri wa Mungu"

Ikiwezekana ni vyema kutotoa maana ya maneno haya waziwazi kwa tafsiri.Wasomi wengi wanaamini muhuri ni alama iliyofanywa kuwatofautisha waumini na wasioamini wakati huu wa dhiki. (Tazama: [[rc:///tw/dict/bible/kt/believe]] and [[rc:///ta/man/translate/figs-explicit]])

<< | >>