sw_tn/rev/02/26.md

36 lines
1.4 KiB
Markdown

# Yule ashindaye
Hii humaanisha mtu yeyote atakayeshinda. "yeyote atakayekataa uovu" au "kwa yule ambaye hatakubali kufanya uovu"
# Atawatawala ... atawavunja vipande
Huu ni utabiri kutoka Agano la Kale kuhusu mfalme wa Israeli, lakini Yesu alimaanisha hapa kwa wale atakaowapa mamlaka juu ya mataifa.
# Atawatawala kwa fimbo ya chuma
Kutawala kwa ukali kunazungumziwa kama kutawala kwa fimbo ya chuma. "Atawatawala kwa ukali kama vile anawapiga na fimbo ya chuma."
# kama mabakuli ya udongo, atawavunja vipande vipande
Kuwavunja katika vipande ni picha inayoonesha 1) kuwateketeza watenda maouvu au 2)kuwashinda maadui. "Atawashinda kabisa maadui wake kama vile kuvunja vipande vipande mabakuli ya udongo."
# Kama nilivyopokea kutoka kwa Baba yangu
Lugha zingine zinaweza kuhitaji kuonesha kilichopokelewa. Maana zinazowezekana ni 1)"Kama vile nilivyopokea mamlaka kutoka kwa Baba yangu" au 2) Kama nilivyopokea nyota ya asubuhi kutoka kwa Baba yangu.
# Baba yangu
Hili ni jina muhimu la Mungu linaloeleza mahusiano kati ya Mungu na Yesu.
# nitampa pia
Hapa inamaanisha yule atakaye shinda.
# nyota ya asubuhi
Hii ni nyota inayoonekana asubuhi kabla ya kupambazuka. Ilikua pia ni ishara ya ushindi.
# Mwenye sikio asikie
Kuwa tayari kusikiliza inazungumziwa kama kuwa na sikio. "Acha ambaye yuko tayari kusikiliza asikilize" au "kama uko tayari kusikiliza, sikiliza"