# Yule ashindaye Hii humaanisha mtu yeyote atakayeshinda. "yeyote atakayekataa uovu" au "kwa yule ambaye hatakubali kufanya uovu" # Atawatawala ... atawavunja vipande Huu ni utabiri kutoka Agano la Kale kuhusu mfalme wa Israeli, lakini Yesu alimaanisha hapa kwa wale atakaowapa mamlaka juu ya mataifa. # Atawatawala kwa fimbo ya chuma Kutawala kwa ukali kunazungumziwa kama kutawala kwa fimbo ya chuma. "Atawatawala kwa ukali kama vile anawapiga na fimbo ya chuma." # kama mabakuli ya udongo, atawavunja vipande vipande Kuwavunja katika vipande ni picha inayoonesha 1) kuwateketeza watenda maouvu au 2)kuwashinda maadui. "Atawashinda kabisa maadui wake kama vile kuvunja vipande vipande mabakuli ya udongo." # Kama nilivyopokea kutoka kwa Baba yangu Lugha zingine zinaweza kuhitaji kuonesha kilichopokelewa. Maana zinazowezekana ni 1)"Kama vile nilivyopokea mamlaka kutoka kwa Baba yangu" au 2) Kama nilivyopokea nyota ya asubuhi kutoka kwa Baba yangu. # Baba yangu Hili ni jina muhimu la Mungu linaloeleza mahusiano kati ya Mungu na Yesu. # nitampa pia Hapa inamaanisha yule atakaye shinda. # nyota ya asubuhi Hii ni nyota inayoonekana asubuhi kabla ya kupambazuka. Ilikua pia ni ishara ya ushindi. # Mwenye sikio asikie Kuwa tayari kusikiliza inazungumziwa kama kuwa na sikio. "Acha ambaye yuko tayari kusikiliza asikilize" au "kama uko tayari kusikiliza, sikiliza"