sw_tn/rev/02/12.md

28 lines
704 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Huu ni mwanzo wa ujumbe wa Mwana wa Adamu kwa malaika wa kanisa la Pergamo.
# Pergamo
Huu ni mji ndani ya Asia ambapo ni Uturuki ya leo.
# upanga mkali, wenye makali kuwili
Hii humaanisha upanga wenye makali mawili, ambao umechongeka pande zote ili kukata pande zote.
# kiti cha enzi cha shetani
Maana zinazowezekana ni 1) nguvu ya Shetani na ushawishi wake juu ya watu, au 2) mahali ambapo Shetani hutawala.
# wewe walishika sana jina langu
Kuwa na imani dhabiti inazungumziwa kama kushikilia kwa nguvu. "Unaniamini kwa dhabiti"
# hukuikana imani yako iliyo kwangu
"Imani" inaweza kutafsiriwa kama kitenzi "kuamini". "hukuacha kuniamini"
# Antipasi
Hili ni jina la mtu.