# Taarifa ya Jumla: Huu ni mwanzo wa ujumbe wa Mwana wa Adamu kwa malaika wa kanisa la Pergamo. # Pergamo Huu ni mji ndani ya Asia ambapo ni Uturuki ya leo. # upanga mkali, wenye makali kuwili Hii humaanisha upanga wenye makali mawili, ambao umechongeka pande zote ili kukata pande zote. # kiti cha enzi cha shetani Maana zinazowezekana ni 1) nguvu ya Shetani na ushawishi wake juu ya watu, au 2) mahali ambapo Shetani hutawala. # wewe walishika sana jina langu Kuwa na imani dhabiti inazungumziwa kama kushikilia kwa nguvu. "Unaniamini kwa dhabiti" # hukuikana imani yako iliyo kwangu "Imani" inaweza kutafsiriwa kama kitenzi "kuamini". "hukuacha kuniamini" # Antipasi Hili ni jina la mtu.