sw_tn/rev/01/09.md

36 lines
1018 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Yohana anaeleza jinsi maono yake yalivyoanza na maelekezo aliyopewa na Roho.
# yenu...nanyi
Hii humaanisha waumini katika makanisa saba
# anayeshiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu thabiti ulio katika Yesu
"aliye na fungu katika ufalme wa Mungu. Ninateseka pia na kuvimilia majaribu pamoja nanyi kwa sababu sisi ni mali ya Yesu"
# kwa sababu ya neno la Mungu
"kwa sababu niliwaambia wengine kuhusu neno la Mungu"
# katika Roho
Yohana anazungumzia kuvutwa na Roho ya Mungu kana kwamba alikua katika Roho. "kushawishika na Roho" au "Roho alinishawishi"
# siku ya Bwana
siku ya kuabudu kwa waumini wa Kristo
# sauti ya juu kama ya tarumbeta
Sauti ilikua na sauti kuu sana ikafanana na tarumbeta
# tarumbeta
Hii humaanisha chombo cha kutengeneza muziki au kuwaita watu kwa ajili ya tangazo au mkutano.
# kwenda Smirna, kwenda Pergamo, kwenda Thiatira, kwenda Sardi, kwenda Philadelphia, na kwenda Laodikia
Haya ni majina ya miji uliko Asia ambayo ni Uturuki ya leo