sw_tn/psa/089/035.md

32 lines
1.2 KiB
Markdown

# Nimeapa kwa utakatifu wangu
Yahwe anatumia utakatifu wake kama msingi wa kiapo chake. Hii ni njia ya kuhakikisha kuwa hakika atafanya alichoahidi kufanya.
# na kiti chake cha enzi kitakuwa kama jua mbele yangu
"na kiti chake cha enzi kitaendelea kama jua mbele yake"
# kiti chake cha enzi
Hapa "kiti cha enzi" kinawakilisha uwezo wa kutawala kama mfalme. Mungu anaahidi kuwa mmoja wa uzao wa Daudi daima atakuwa mfalme.
# kama jua mbele yangu
Mungu anafananisha utawala wa Daudi kama mfalme na jua kusisitiza kuwa mtu kutoka uzao wa Daudi atatawala daima kama mfalme.
# kitaimarishwa milele
Hapa kinachozungumziwa ni kiti cha enzi au uwezo wa kutawala kama mfalme. "nitakisababisha kudumu milele"
# milele kama mwezi
Mungu anafananisha utawala wa Daudi kama mfalme na mwezi kusisitiza kuwa mtu kutoka uzao wa Daudi atatawala daima kama mfalme.
# mwezi, shahidi wa uaminifu wa angani
Mwezi unazungumziwa kana kwamba ni mtu anayeshuhudia Mungu akifanya ahadi yake kwa Daudi. "mwezi, ambao ni kama shahidi mwaminifu aliye angani"
# Sela
Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.