# Nimeapa kwa utakatifu wangu Yahwe anatumia utakatifu wake kama msingi wa kiapo chake. Hii ni njia ya kuhakikisha kuwa hakika atafanya alichoahidi kufanya. # na kiti chake cha enzi kitakuwa kama jua mbele yangu "na kiti chake cha enzi kitaendelea kama jua mbele yake" # kiti chake cha enzi Hapa "kiti cha enzi" kinawakilisha uwezo wa kutawala kama mfalme. Mungu anaahidi kuwa mmoja wa uzao wa Daudi daima atakuwa mfalme. # kama jua mbele yangu Mungu anafananisha utawala wa Daudi kama mfalme na jua kusisitiza kuwa mtu kutoka uzao wa Daudi atatawala daima kama mfalme. # kitaimarishwa milele Hapa kinachozungumziwa ni kiti cha enzi au uwezo wa kutawala kama mfalme. "nitakisababisha kudumu milele" # milele kama mwezi Mungu anafananisha utawala wa Daudi kama mfalme na mwezi kusisitiza kuwa mtu kutoka uzao wa Daudi atatawala daima kama mfalme. # mwezi, shahidi wa uaminifu wa angani Mwezi unazungumziwa kana kwamba ni mtu anayeshuhudia Mungu akifanya ahadi yake kwa Daudi. "mwezi, ambao ni kama shahidi mwaminifu aliye angani" # Sela Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.