sw_tn/psa/089/019.md

28 lines
970 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Mwandishi anachukulia kuwa msomaji anafahamu historia ya jinsi Daudi alivyochaguliwa kuwa mfalme.
# Nimeweka taji kwa aliye hodari
Kuweka taji juu ya kichwa cha mtu ni ishara ya kumfanya kuwa mfalme. "Nimemfanya mtu hodari kuwa mfalme"
# Nimeweka taji kwa aliye hodari
Tafsiri zingine za Biblia zina "kumpa nguvu aliye hodari" au "kumsaidia aliye hodari."
# Nimemwinua mmoja niliyemchagua miongoni mwa watu
Hapa "nimemwinua" inamaanisha kuchagua. Inadokezwa kuwa Mungu alimchagua mtu huyu kuwa mfalme. "Nimemchagua mmoja miongoni mwa watu kuwa mfalme"
# kwa mafuta yangu matakatifu nimempaka
Hapa kumwaga mafuta juu ya kichwa cha mtu ni ishara kuwa Mungu anamchagua huyo mtu kuwa mfalme.
# Mkono wangu utamshika; mkono wangu utamtia nguvu
Hapa "mkono" unamaanisha nguvu na mamlaka ya Yahwe. "nitamshika na kumfanya kuwa na nguvu"
# mwana wa uovu
Mwandishi anawazungumzia wale wenye sifa au tabia ya uovu kama "wana wa uovu." "mtu mwovu"