# Taarifa ya Jumla: Mwandishi anachukulia kuwa msomaji anafahamu historia ya jinsi Daudi alivyochaguliwa kuwa mfalme. # Nimeweka taji kwa aliye hodari Kuweka taji juu ya kichwa cha mtu ni ishara ya kumfanya kuwa mfalme. "Nimemfanya mtu hodari kuwa mfalme" # Nimeweka taji kwa aliye hodari Tafsiri zingine za Biblia zina "kumpa nguvu aliye hodari" au "kumsaidia aliye hodari." # Nimemwinua mmoja niliyemchagua miongoni mwa watu Hapa "nimemwinua" inamaanisha kuchagua. Inadokezwa kuwa Mungu alimchagua mtu huyu kuwa mfalme. "Nimemchagua mmoja miongoni mwa watu kuwa mfalme" # kwa mafuta yangu matakatifu nimempaka Hapa kumwaga mafuta juu ya kichwa cha mtu ni ishara kuwa Mungu anamchagua huyo mtu kuwa mfalme. # Mkono wangu utamshika; mkono wangu utamtia nguvu Hapa "mkono" unamaanisha nguvu na mamlaka ya Yahwe. "nitamshika na kumfanya kuwa na nguvu" # mwana wa uovu Mwandishi anawazungumzia wale wenye sifa au tabia ya uovu kama "wana wa uovu." "mtu mwovu"