sw_tn/psa/073/008.md

20 lines
680 B
Markdown

# Taarifa ya Ujumla:
Asafu anaendela kueleza ambavyo wakati mwingine anataka kulalamika kwa Mungu kuhusu wale ambao wana "kiburi" na "waovu".
# Hudhihaki
Yule ambaye wanamdhihaki inaweza kuelezwa vizuri. "Wanamdhihaki Mungu na watu wake"
# Wanaweka mdomo wao dhidi ya mbingu
Hapa neno "mbingu" ni njia nyingine ya kusema Mungu, ambaye anaishi mbinguni. "wanazungumza dhidi ya Mungu aliye mbinguni"
# Wanaweka mdomo wao
"kuzungumza vikali" au "kuzungumza na kusudi"
# ulimi wao unatembea duniani
Neno "ulimi" ni njia nyingine ya kusema watu wenyewe. Maana zinazowezekana ni 1) "wanaenda duniani wakisema mambo mabaya kumhusu Mungu" au "wanaenda kila mahali na kujisifia."