sw_tn/psa/067/001.md

24 lines
697 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.
# Kwa mwanamuziki mkuu
"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"
# kwenye vyombo vya nyuzi
"watu wanapaswa kucheza vyombo vya nyuzi na wimbo huu"
# kusababisha uso wake ung'ae kwetu
Mwandishi anamzungumzia Yahwe kuwatendea fadhila kana kwamba uso wa Yahwe uling'aa mwanga juu yao. "kututendea fadhili"
# njia zako zijulikane duniani
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watu wajue njia zako duniani"
# wokovu wako miongoni mwa mataifa yote
Mwandishi anatamani kila mtu ajue kuwa Mungu ana uwezo wa kuwaokoa. Hii inaweza kuwekwa wazi. "na watu wa mataifa yote wajue kuwa una uwezo wa kuwaokoa"